WANAWAKE WALIO ZAA CHINI YA UMRI WA MIAKA 18 WAELEZEA JINSI WALIVYO PAMBANA NA CHANGAMOTO KATIKA MAISHA
Kikundi cha akina mama ambao wamezaa chini ya umri wa miaka 18 wanaoishi mtaa wa mtwivila wamepania kujikwamua kiuchumi kwa kuchangiana sh.2000 kila wanapo kutana ili kuweza kufungua mgahawa na hatimaye kuweza kuwasaidia kuwalea watoto wao.
Akizungumza kwa niaba ya wanamama wenzie jane ambaye pia ana anamtoto mwenye umri wa miaka 5 amesema kuwa lengo la kuanzishwa kwa kikundi hicho ni kutaka kuwasaidia akina dada ambao wanazaakatika umri mdogo na kutelekezwa kuweza kujikwamua kiuchumi kwa kupata kiasi cha fedha kutoka katika kikundi hicho.
Aidha mwenyekiti wa kikundi hicho amesema kuwa wanatarajia kuanzisha mgahawa japo wanakabiliwa na changamoto ya kukosa fedha.
ENDELEA KUFUATILIA MATUKIO YA PICHA KUHUSU ZIARA YA UMATI KWA VIJANA KATIKA MANISPAA KUHUSU NA MWANASAIKOLOJIA WA MAMBO YA KIJAMII
No comments:
Post a Comment