Na denis nyali
Katika kutatua tatizo la
ajira linaloendelea hapa nchini kituo cha vijana UMATI wakishirikiana na AMREFU
hii leo wameendesha semina ya ujasiliamali kwa vijana ili kuweza kufahamu fulsa
zilizopo kwa kuzitumia na kujikwamua kiuchumi.
Akizungumza na overcomers fm
radio mratibu wa mradi wa afya ya kijana ni haki tuitete bi. Matha kisweka
amesema kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo vijana kutambua fulsa
zinazo wazunguka na kuzitendea kazi.
Aidha amesema kuwa vijana hapa nchini wanakabiliwa
na chanagamoto kubwa ya ukosefu wa ajira hivyo kupitia mafunzo hayo vijana
wataweza kujipatia fulsa za kujikwamua kwa kupitia mikopo inayo tolewa na
taasisi mbalimbali hapa nchini
Mafunzo hayo ya ujasiliamali
yanatolewa kwa siku mbili katika kituo cha vijana umati huku vijana zaidi ya 50
kutoka katika kata sita manispaa ya iringa na wale wa nje ya manispaa wakishiriki.
Kwa upande wao vijana
walioshiriki mafunzo hayo wamekipongeza kituo cha vijana UMATI pamoja na Amrefu
kwa kutambua umhimu wa elimu ya ujasiliamali kwa vijana na kuahidi kuitumia
elimu hiyo ipasavyo.
No comments:
Post a Comment