Friday, September 27, 2013

                                   habari na denis nyali

Vijana wametakiwa kujitokeza kupima na kujua afya zao ili kuishi maisha ya kujiamini katika kukamilisha ndoto zao
Akizungumza wakati wa siku ya maadhimisho ya siku ya ukimwi yaliyoandaliwa na shule ya sekondari lugalo wakishirikiana na kituo cha vijana umati mratibu wa  kituo cha umati amesemakuwa lengo la maadhisho hayo ni kuwahabarisha vijana kuhusu afya ya uzazi habari burudani na upimaji wa hiari wa virusi vya ukimwi.
maadhimisho hayo yamehudhuliwa na wadau mbalimbali akiwemo dr.bonaventura kalumbete ambaye ni mratibu wa kudhibiti ukimwi idara ya afya manispaa ya Iringa

Dr.kalumbete ameeleza historia ya ukimwi na kusema kuwa  kwa mara ya kwanza ukimwi uligunduliwa marekani mwa 1980 na Tanzania 1983 ambapo kwa takwimu za 2003-2004 na kuendelea  maambukizi kitaifa yalikuwa asilimia 7 lakini kwa sasa maambukizi yamepungua hadi kufikia asilimia 5 kitaifa hivo amewasihi wanafunzi na jamii kwa ujumla kuwa makini na gonjwa hili ambalo hadi sasa hakuna chanjo wa tiba yake.
Kwa upande wake mkuu wa shule Mwl. Kabungu amewashukuru wadau wote wa afya kwa kuileta huduma hiyo kwa wanafunzi na kuwasihi wanafunzi kuwa makini kusikiliza kile watakachofundisho bila kusahau kutambua afya yao.
Mratibu wa mradi wa haki ya kijana ni haki tuitete matha kisweka akitoa maelezo juu ya mradi jinsi unavyofanya kazi yake
       KITUO CHA VIJANA UMATI PAMOJA NA LUGALO SECONDARI VYAADHIMISHA SIKU YA UKIMWI KWA KUTOA HUDUMA ZA UPIMAJI NA WA VVU, BURUDANI, NA USHAURI NA NASIHI PAMOJA NA ELIMU NA HABARI.
 

 Baadhi ya Umati wa wanafunzi wa shule ya sekondari lugalo waliohudhuria katika maadhimisho ya siku ya ukimwi lugalo.
Rais wa umati  akitoa burudani kwa wanafunzi waliofika katika maadhimisho hayo.

Thursday, September 19, 2013

UMATI PAMOJA NA AMREFU WAENDELEA KUTOA SEMINA KWA VIJANA KUHUSU MAMBO YA UJASILIAMALI KATIKA KITUO CHA UMATI MTWIVILA IRINGA.





Mwezeshaji Bi. Dora  akiendelea na darasa katika ukumbi wa kituo cha vijana UMATI.



           IRINGA
              Na denis nyali

Katika kutatua tatizo la ajira linaloendelea hapa nchini kituo cha vijana UMATI wakishirikiana na AMREFU hii leo wameendesha semina ya ujasiliamali kwa vijana ili kuweza kufahamu fulsa zilizopo kwa kuzitumia na kujikwamua kiuchumi.

Akizungumza na overcomers fm radio mratibu wa mradi wa afya ya kijana ni haki tuitete bi. Matha kisweka amesema kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo vijana kutambua fulsa zinazo wazunguka na kuzitendea kazi.

Aidha  amesema kuwa vijana hapa nchini wanakabiliwa na chanagamoto kubwa ya ukosefu wa ajira hivyo kupitia mafunzo hayo vijana wataweza kujipatia fulsa za kujikwamua kwa kupitia mikopo inayo tolewa na taasisi mbalimbali hapa nchini

Mafunzo hayo ya ujasiliamali yanatolewa kwa siku mbili katika kituo cha vijana umati huku vijana zaidi ya 50 kutoka katika kata sita manispaa ya iringa na wale wa nje ya  manispaa wakishiriki.

Kwa upande wao vijana walioshiriki mafunzo hayo wamekipongeza kituo cha vijana UMATI pamoja na Amrefu kwa kutambua umhimu wa elimu ya ujasiliamali kwa vijana na kuahidi kuitumia elimu hiyo ipasavyo.

 


Wednesday, September 18, 2013

PICHA YA BAADHI YA VIJANA WAKIWASILISHA FULSA AMBAZO ZIPO NDANI YA JAMII

 KATIKA MAKUNDI.





 KITUO CHA VIJANA UMATI  KUENDESHA MAFUNZO YA UJASILIAMALI ILI KUWAJENGEA VIJANA UWEZO WA KUJIKWAMUA KIUCHUMI KUTOKANA NA KIASI CHA PESA KIDOGO WANAZOZIPATA.

                        ENDELEA KUTAZAMA MATUKIO YA PICHA.
Afisa vijana  Manispaa Haruna Yassini akitoa maelekezo ya namna ya kushiriki katika mafunzo ya ujasiliamali
 
Mwezeshaji wa mafunzo dola Myinga Akiendelea kutoa mafunzo
 
 
Baadhi ya washiriki wakisikiliza kwa makini mafunzo hayo
 

Saturday, September 7, 2013

                  HABARI PICHA KUTOKA KATIKA KATA YA MKWAWA

Mmoja kati ya vijana kutoka kata ya mkwawa akizungumzia changamoto zinazo wahusu vijana wa kata hiyo

 Picha ya pamoja na akina dada waliozaa chini ya umri wa miaka 18





     WANAWAKE WALIO ZAA CHINI YA UMRI WA MIAKA 18 WAELEZEA JINSI WALIVYO PAMBANA NA CHANGAMOTO KATIKA MAISHA

Kikundi cha akina mama ambao wamezaa chini ya umri wa miaka 18 wanaoishi mtaa wa mtwivila wamepania kujikwamua kiuchumi kwa kuchangiana sh.2000 kila wanapo kutana ili kuweza kufungua mgahawa na hatimaye kuweza kuwasaidia kuwalea watoto wao.

Akizungumza kwa niaba ya wanamama wenzie jane ambaye pia ana anamtoto mwenye umri  wa miaka 5 amesema kuwa lengo la kuanzishwa kwa kikundi hicho ni kutaka kuwasaidia akina dada ambao wanazaakatika umri mdogo na kutelekezwa kuweza kujikwamua kiuchumi kwa kupata kiasi cha fedha kutoka katika kikundi hicho.

Aidha mwenyekiti wa kikundi hicho amesema kuwa wanatarajia kuanzisha mgahawa japo wanakabiliwa na changamoto ya kukosa fedha.

ENDELEA KUFUATILIA MATUKIO YA PICHA KUHUSU ZIARA YA UMATI KWA VIJANA KATIKA  MANISPAA KUHUSU NA MWANASAIKOLOJIA WA MAMBO YA KIJAMII








SEMINA YA UFUATILIAJI KWA VIJANA WENYE MATATIZO YA KISAIKOLOJIA NA WALE WALIOKUWA WAMEATHIRIKA NA MDAWA YA KULEVYA,MIMBA ZA UTOTONI,MAAMBUKIZI YA MAGONJWA YA ZINAA





Kituo cha UMATI hii leo kinatarajia kufanya semina ya ufuatiliaji kwa vijana wenye matatizo ya kisaikolojia na kama vile madawa ya kulevya ,mimba za utotoni ,na wale wanaoisahi na virusi vya ukimwi.

        SHUHUDA KUTOKA KWA VIJANA WALIO PATA MAFUNZO NA YAMEWASAIDIA

      
Petro mwenye tisheti nyeusi kijna ambaye aliwahi kuvuta bangi kwa miaka miwili na kuugua ugonjwa wa gonolea lakini baada ya ushauri na tiba kutoka kituo cha vijana UMATI amepona na yupo safi kabisa leo hii ameshuhudia



                    Baadhi ya vijana waliohudhuria katika semina hiyo



Wa kwanza kushoto ni rashidi kijana ambaye kutoka na kukosa ajira akaamua kujiingiza kwenye tabia ya udokozi lakini baada ya kupata ushauri kutoka UMATI ameweza kubadilika na pia alikuwa akisumbuliwa na magonjwa ya ngono na sasa amepona kabisa kupitia kituo cha UMATI
Fuatilia matukio ya picha sasa kupitia mtandao huu wa vijana