Vijana wametakiwa kujitokeza kupima na kujua afya zao ili kuishi maisha ya kujiamini katika kukamilisha ndoto zao
Akizungumza wakati wa siku ya maadhimisho ya siku ya ukimwi yaliyoandaliwa na shule ya sekondari lugalo wakishirikiana na kituo cha vijana umati mratibu wa kituo cha umati amesemakuwa lengo la maadhisho hayo ni kuwahabarisha vijana kuhusu afya ya uzazi habari burudani na upimaji wa hiari wa virusi vya ukimwi.
maadhimisho hayo yamehudhuliwa na wadau mbalimbali akiwemo dr.bonaventura kalumbete ambaye ni mratibu wa kudhibiti ukimwi idara ya afya manispaa ya Iringa
Dr.kalumbete ameeleza historia ya ukimwi na kusema kuwa kwa mara ya kwanza ukimwi uligunduliwa marekani mwa 1980 na Tanzania 1983 ambapo kwa takwimu za 2003-2004 na kuendelea maambukizi kitaifa yalikuwa asilimia 7 lakini kwa sasa maambukizi yamepungua hadi kufikia asilimia 5 kitaifa hivo amewasihi wanafunzi na jamii kwa ujumla kuwa makini na gonjwa hili ambalo hadi sasa hakuna chanjo wa tiba yake.
Kwa upande wake mkuu wa shule Mwl. Kabungu amewashukuru wadau wote wa afya kwa kuileta huduma hiyo kwa wanafunzi na kuwasihi wanafunzi kuwa makini kusikiliza kile watakachofundisho bila kusahau kutambua afya yao.